Vipi ukipata simu ambayo inakaa na chaji kwa muda mrefu, huwenda ikawa ni furaha ya kudumu kwako.
Basi fahamu kuwa kampuni ya ''Energizer'' imekuja na aina mpya ya simu yenye uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa siku 50
Simu hiyo inatajwa kuwa na betri yenye uwezo wa (18,000 mAh) huku betri yenye uwezo mkubwa kwa sasa kwenye simu za mkononi inatajwa kufikia 6000mAh
mAh ndiyo kipimo cha uwezo wa betri ya simu, mAh ni kifupi cha ‘’milliampere-hour’’ ambayo inatumika kupima uwezo wa betri kwa muda fulani,
Picha: Energizer