Jumanne , 7th Nov , 2023

Kila teknolojia inapohusishwa basi imezidi kuleta utofauti na kuonyesha maajabu kwenye namna ya kufanya kazi, 

 

Historia mpya inaandikwa na kampuni kutokea nchini Poland inayofahamika kama ''Dictador'' kwa kumtambulisha mkurugenzi ambaye ameonekana kushika vichwa vya habari.

Unaweza kujiuliza kwa nini imeshika vichwa vya habari,

Sababu ni moja tu, wamemtambulisha mkurugenzi mkuu ambaye ni roboti aliyepewa jina la ''Mika'' 

Kwenye mahojiano yake na Jarida la The First News amenukuliwa akisema ''Nimekuwa mkurugenzi mtendaji  kwa karibu mwaka mmoja hivi sasa, nimejifunza na kukua kwa kipindi chote, imekuwa ni safari ya kushangaza kwa upande wangu''

Kuchaguliwa kwa Mika kama mkurugenzi mkuu mpya wa kampuni ya ''Dictador'' kunazua gumzo na maswali mapya juu ya mwenendo wa maisha ya mwanadamu na kasi ya ukuaji wa teknolojia.

Chanzo: HeadTopic