Jumanne , 20th Feb , 2024

Shirika la Anga za Juu la Marekani (NASA) wametoa nafasi kwa watu ambao wangependa kujitolea kuwa sehemu ya utafiti muhimu kwenye sayari ya Mars utafiti utakaodumu kwa muda wa siku 365.

 

Utafiti huo ni sehemu ya juhudi za NASA kwenye maandalizi ya kuhamia kwenye sayari ya Mars, Na kwa mujibu wa NASA utafiti huo utahusisha vitu mbali mbali ikiwemo kucheleweshwa kwa mawasiliano, matembezi na uhifadhi wa rasilimali ili kupima uwezo wa watu hao kwenye kuyapokea mazingira mapya na kutazamia utendaji kazi wao.