Picha kubwa ni bustani ya maua, picha ndogo ni gari aina ya Spacio
"Tangu mdogo nilikuwa napenda maua, nilikuwa na gari yangu ya Spacio nikaiuza kwa milioni 5 ila pesa yote nikaaingiza kwenye garden, hicho kitu ndiyo kikanituliza nyumbani na nitayapanda mpaka nizeeke" amesema Hawa Mniga
Aidha akaendelea kusema "Mimi siuzi maua ila napenda kuona nyumba yangu ikiwa hivyo, uzuri wake yanazaa unaweza ukanunua ua moja kwa shilingi elfu sabini ila baada ya miezi kama saba linatoa watoto, kwa hiyo wale watoto utawauza kutokana na size kuna ya elfu 30 au elfu 25".
Show hiyo ya DADAZ huruka hewani kupitia East Africa TV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 5:00 Asubuhi hadi 6:00 Mchana ambapo huwa kuna wageni mbalimbali kama watu wa taaluma, lifestyle, familia, mahusiano na burudani.