
Mwanaharakati wa Mtandao wa Jinsia Vivian Lugulumu
Akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, kinachoruka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 12:00 asubuhi mpaka 4:00 asubuhi, Mwanaharakati huyo amesema sasa hivi ndoa imefanywa kama fashion kwa wanaoenda kuolewa au kuoa.
"Mahari ni kwa ajili ya wanawake bikra na wanaume bikra tu, ila kwa sasa ndoa ndiyo imefanywa kama fashion kwa wanawake wanavyoenda kuolewa, kwanza mkaja wa mama na mahari ni vitu viwili tofauti, mkaja ni ahsante kwa mama kwa kumlea binti yake" amesema Vivian Lugulumu.