Ijumaa , 3rd Nov , 2023

Kisakuzi kinachosifika kwa kulinda faragha za mtumiaji wake na kuzuia kila aina ya matangazo pindi mtumiaji anapotumia ''Brave'' umekuja na jambo jipya kwa watumiaji wake,

 

Brave kwenye kuendenda na kasi ya ulimwengu wa Teknolojia na yenyewe kwa sasa imetambulisha teknolojia ya akili mnepe ambayo itakuwako ndani ya kisakuzi hicho, na hii ni kama ChatGPT ya Open.ai, Bing ya Microsoft, Bard ya Google lakini huku ndani ya Brave inafahamika kama ''Leo'' itamke Lio

Hii ''Leo'' kwa mujibu wa waendeshaji wa kisakuzi cha Brave wanaitaja kuwa ni moja kati ya akili mnepe ambayo ni tofauti na yenye ubora kuwahi kutokea, moja ya sifa ambazo zimeorodheshwa kuhusu ''Leo''

- Inauwezo wa kufanya tafsiri.

- Inauwezo wa kukupa majibu kwa mwaswali utakayo uliza.

- Inaweza kufupisha makala iliyoandikwa kwa urefu na kumrahisishia msomaji wake. 

- Inauwezo wa kukupa mawazo mapya kwa kubuni maudhui.

- Haikusanyi taarifa za mtumiaji wake.

- Haina haja kujiunga ili kuitumia.

 

Lakini hii itapatikana kwa watumiaji waonaotumia kwenye tarakilishi zilizo na uwezo kuanzia ''version 1.60'' hivyo ni vyema kufanya maboresho kupata huduma ya ''Leo''

Pia kwenye ''Premium version'' ya ''Leo'' itamuhitaji mtumiaji kulipia kiasi cha shilingi elfu 37,500 kwa pesa za ki-Tanzania, hii pia ni sawa na ''chatGPT 4'' ambayo kwa mwezi ili uweze kuitumia utahitajika kulipia kiasi cha shilingi 50,000 kwa pesa ya ki-Tanzania.

Lakini mtazamo wetu kama SUPATECH kwenye akili mnepe zote ambazo zimetoka kwenye kipindi cha hivi karibuni ''Bing'' kutoka kwenye kampuni ya ''Microsoft'' inazidi kuwa bora kwani hii ndiyo teknolojia pekee ya akili mnepe inayotoa majibu hata yanayohusisha matukio ya kipindi cha hivi karibuni.

Tunaposema matukio ya hivi karibuni tunamaanisha kile kinachoendelea kwa muda huu, mfano OPEN.AI imewezeshwa kufahamu taarifa ambazo zinaishia mwaka 2021 pekee kwa miaka mingine kama 2023 haina majibu kuhusiana na kinachoendelea.

Picha: Verge