
Msanii na Diwani Baba Levo
Baba Levo amesema Magereza ambayo yanapatikana nje ya Dar yanakuwa na kazi ngumu za kilimo siku nzima, hali ambayo hata yeye alikutana nayo alipohukumiwa kifungo cha miezi mitano jela.
Akipiga stori kupitia show ya Friday Night Live ya East Africa TV, Baba Levo amesema "Nilivyofungwa jela miezi mitano nikakata rufaa, baada ya kufanya hivyo wakaniambia natakiwa niende tena gerezani kwa muda wa mwaka mmoja na siku mbili jambo ambalo lilinipa mawazo sana"
Aidha Baba Levo ameongeza kusema "Tofauti ya jela za Dar Es Salaam na nje ya Dar ni kazi za kilimo, kwa hiyo hata mimi nilivyofungwa kule Kigoma nilikuwa nafanya kazi ngumu sana za kilimo, magereza ya nje ya Dar ni magumu sana"