Jumatatu , 24th Oct , 2016

Msanii wa filamu nchini Rammy Galis amesema pengo aliloacha msanii wa filamu nchini marehemu Steven Kanumba ni kubwa na halitazibika litabakia kuwa hivyo.

Rammy Galis (Kushoto) Steven Kanumba (Kulia)

 

Galis ameyasema hayo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, ambapo alikuwa akijibu maswali mbalimbali ya mashabiki.

“Mchango wa Kanumba ni mkubwa sana na pengo lake litabakia kuwa hivyo na mimi nilifanikiwa kufanya naye kazi mwishoni mwishoni kabla ya mauti kumkumba alikuwa ni mtu wa aina yake” Amesema Galis

Aidha Galis amesema wasanii wa filamu nchini wanatakiwa kubadilika kulingana na matukio yanayofanyika katika jamii na kuepuka kufanya uigizaji wa zamani wa kuzunguka na magari na kukaa sebuleni kwenye makochi.

Pamoja na hayo Galis amesema mwezi Desemba mwaka huu anatarajia kuachia filamu aliyoigiza na waigizaji wa Nigeria na kuwataka wadau kukaa mkao wa kula kuburudika na kazi yake kwani imeandaliwa kwa viwango vya kimataifa.

Tags: