Klabu ya Simba inashida ya uwepo wa Mchezaji anayeweza kucheza kwa kutokea pembeni ambaye anaweza kufunga na kutengeneza magoli.Viungo wa pembeni wa timu ya Simba wanachangamoto ya kutengeneza nafasi Kibu Denis,Radack Chasambi,Edwin Balua,Joshua Mutale wote mchango wao wa kufunga na kutengeneza nafasi umekuwa mdogo msimu huu.
Simba SC yenyewe itaingia uwanjani siku ya Jumamosi ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya FC Bravos ya kutokea Angola kwenye mchezo wa kwanza wa makundi uliochezwa uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam.