
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mziwanda ameposti picha mbili tofauti, kila moja ikiwa na ujumbe mzito unaoonesha namna Chino amekuwa msaada mkubwa kwake......"Moja ya kitu Ambacho Dunia Hawajui Una upendo na kuthamini cha Mtu au hisia za Mtu. ‘Kiukweli unaniheshimisha japo ni Kaka yako Ila you are My boss. Nakuombea Ubaki Kua Boss of all time. Wana Man Gang. Can’t wait to sign''
Ujumbe huu unaonesha wazi kuwa licha ya ukaribu wao wa kifamilia, Nuh anamchukulia Chino kama mtu wa muhimu sana katika maisha yake ya kazi na faragha, hadi kufikia kumuita boss wake, Katika picha ya pili, ambapo anaonekana akiwa amevaa t-shirt nyeupe na kofia, Nuh alieleza......"Wewe anza kunisema Ila Roho ina Amani. Thanks My Boss Chino Kidd Asante Pia kwa Apartment ya kuishi Chino Kidd. Ngoma zinakuja
Ujumbe huu unaashiria kuwa mbali na kumpatia sehemu ya kuishi, Chino Kidd pia amehusika moja kwa moja katika kuandaa kazi mpya ya muziki ambayo huenda ikatoka siku za hivi karibuni,Kuna matarajio makubwa ya wimbo mpya kutoka kwa wawili hawa, na mashabiki wa Bongo Fleva tayari wameonesha hamu ya kuusikia.