
Pichani Mr Blue na Kalapina
"Mimi ndio dogo pekee niliyekuwa naweza kwenda Kikosi cha mizinga nikakaa na wasinifanye chochote navaa hereni ubishoo nini nawasalimia mabrother na hawanizingui Kwahiyo mimi ni mzaliwa wa mjini hapa hapa mimi Dully Sykes ananijua kabla sijatoka kimuziki'' Amesema Blue
"Kuna watu waliandika kwenye gazeti "Kalapina anataka kumuoa Mr Blue ,Kalapina ilimuumiza sana kwasababu tulikuwa tunakutana naye kila siku na mapambano yangu anayaona na akiona muziki wangu na mimi ni vitu tofauti akawa ananiambia wewe na muziki wako ni vitu tofauti" Amesema Blue
"Unaimba kuhusu ubrothermen lakini wewe sio brothermen kwahiyo Kalapina alitamani pia watu wajue kuwa mimi sio brothermen kama ambavyo muziki wangu unaonekana'' Amesema Blue
"Kalapina alinitafuta tukakaa chini akaniambia twende tuwafungulie mashitaka haki za binadamu na tulienda kabisa yeye ndio alikuwa amekasirika kwanini wameandika nataka nimuoe mdogo wangu wakati mimi namuheshimu?'' Amesema Blue
"Changamoto tu kipindi kile mmi nilikuwa bado mdogo na umaarufu mwingi sikutaka kufuatilia mambo hayo nawaza kula bata tu nikamwambia Brother achana nao washamba tu kwahiyo mpaka leo tunaheshimiana sana" Amesema Blue