YOUNG KILLER
Hivi karibuni Prodyuza Mona Gangster aliiambia eNewz kuwa wasanii aliokuwa akidili nao walijisahau na kuvimba kichwa na umarufu ulipo mzidi Young Killer akawa hashikiki hali ilisababisha hadi kuvunja makubaliono waliyokuwa wamewekeana.
eNewz imekutana na Young Killer na kuweka wazi juu ya tuhuma hizo lakini Killer alikanusha kauli ya Mona Gangster kuwa ustaa ulimzidi na kusema yeye alikuwa staa hata kabla ya kuja Dar alikuwa staa tangu akiwa Mwanza.
Hata hivyo Young Killer aliiambia eNewz kuwa Mona Gangstar anamchango katika mziki wake lakini kuna masuala ambayo hayakuwa sawa kwa upande wa malipo na jinsi ya kugawana kile ambacho kinakuwa kinapatikana katika kazi zao.
Young Killer ameendelea kusisitiza kuwa yeye ustaa haujambadilisha chochote na hapo awali alikuwa akifanya muziki kama kitu cha ziada katika maisha yake yeye ndoto zake zilikuwa kuwa Sheikh ama Ustadhi katika Misikiti kwani alipenda saana kusoma Quruan.

