Picha ya Drake na Jay Z
Line hiyo ya Jay Z inasema “Drake jinsi watakujia kwa uhasama wa kipuuzi na kujaribu kukuvuruga kwa kujificha, waangalie wasaliti. Nimeyaona yote na nimefanya yote”.
Miaka 6 baadaye 2017 Drake ali-release Album ya More Life na ndani yake kuna ngoma ya ‘Free Smoke’ akimjibu Jay Z kwanini hakuchukua ushauri wake huo
“Sikumsikiliza Hov kwenye wimbo huo wa zamani aliponiambia nisijali, nimepata kuridhika zaidi ya kichwa chako. Na nimeona wote mkipotea na wengi wenu kufa”.
JayZ kama aliona mbali kuhusu bifu za Drake lakini Drizzy kama amekaidi ushauri huo kwa sababu mpaka sasa amekuwa kwenye bifu na baadhi ya rappers kama Pusha T, Kanye West, Joe Budden, Tyga, Kendrick Lamar na Future.