Jumanne , 12th Oct , 2021

Wimbo wa “Essence Remix” wa Wizkid akiwa na Tems na Justin Bieber umeingia katika Top 10 ya chat za Billboard Hot 100 na kuweka record ya kuwa wimbo wa kwanza wa Afrobeat kuingia katika Top 10 ya chat hizo.

Picha ya wasanii Justin Bieber (kushoto), Tems (katikati) na Wizkid (kulia)

Wimbo huu ukiwa na wiki 14 katika Billboard Hot 100 umepanda kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 11 wiki iliyopita.

“Essence” imepata airplay ya Radio na TV mara million 48.9 wiki iliyopita kwa nchini Marekani, na streams million 11.2 katika digital platforms.