Ijumaa , 12th Jun , 2015

Msanii wa miondoko ya Bongofleva nchini Witnesz The Fitness ambaye hivi karibuni alipatwa na maswahiba nyumbani kwake eneo la Kijitonyama ameamua kuongea na mashabiki wake juu ya mipango ambayo aliyonayo kwa sasa.

msanii wa muziki Witnesz The Fitness akiwa na mgeni pamoja na mchumba wake Ochu sheggy

Staa huyo aliyeibiwa vitu mbalimbali vikiwemo Laptops, simu na vifaa vya utayarishaji pamoja na jumla ya dola za kimarekani elfu tatu, amesema kuwa licha ya hasara hiyo kubwa lakini hatoacha kuendelea na mipango yake katika muziki.

Witnesz na mpenzi wake Ochu Sheggy hivi sasa wamewaeleza mashabiki wao kuwa walipanga kutoa baadhi ya nyimbo zao mpya ikiwemo yake Witnesz iitwayo 'Buku Jero' na ya Ochu inayoitwa 'Dumange' ambapo staa huyo ameongea na eNewz kuhusiana na project mpya ya mchumba wake Ochu ambayo inatarajiwa kuachiwa rasmi siku ya jumapili.