Jumanne , 10th Mei , 2022

Madam Wema Sepetu ameonesha kutopendezwa na Bob Junior kusema yeye ni mwanamke wake na anataka kumtolea posa kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Picha ya Wema Sepetu na Bob Junior

Wema amekanusha madai ya taarifa hiyo baada ya kushea ujumbe ufuatao

"Niko disappointed na Bob Junior sana cause maisha yangu always nimekuwa nikimchukulia as a friend na nimekuwa nikimkubali kama mwana, sasa sielewi ndugu yangu ukala nini au umeona ni sawa kwenda kuongea kuwa mimi ni mwanamke wako?”.

"Nimekuwa sad saaaaanaaa maana hata sielewi namwambiaje Mwanaume wangu akanielewa.Kiukweli umenikosea sana haya posa hiyo ya wapi au ulikuwa umelewa, yaani kuna vitu vinakera sana kwa kweli"