shindano la kucheza muziki la Dance100% 2014
Kundi hilo lenye umachachari wa kusakata dansi, katika mahojiano yake na eNewz likajinadi kwa mashabiki wao namna lilivyojipanga ili kuhakikisha kuwa wao ndio wanaibuka washindi wa shindano hilo.
Siku zinaendelea kwisha, na macho yote ni kuelekea fainali za mashindano haya jumamosi hii, swali lenye uzito wa kutosha likibaki kuwa ni kundi litakalochomoka na mpunga milioni 5 kati ya The WT, Wakali sisi, Best Boys, Wazawa Crew na The winners Crew.