Jumanne , 29th Jul , 2014

Ikiwa leo waislam kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wanaungana kusherekea kwa pamoja Sikukuu ya Eid El Fitr baada ya kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

wasanii Mwasiti na Shetta wa Tanzania

Kutoka tasnia ya burudani nchini, wasanii mbalimbali wametoa salamu zao za Eid kwa mashabiki wao katika kuitia nakshi siku hii kubwa.

Mbali na salamu mbalimbali kwa njia ya mitandao ya kijamii, kupitia eNewz, wakali wa Bongofleva Nurdin Bakari, Mwasiti Almasi, AT kati ya wengine, wamewataka Waislam na mashabiki wao kwa ujumla kusherekea siku hii kwa kutenda mema, kukumbuka wenye hali ngumu na kujiepusha na shari.

Hii yote ni katika kutia nakshi siku hii kubwa, na eNewz tunawatakia waislam wote Eid Mubarak.