Jumanne , 24th Mar , 2026

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Elie Mpanzu (Kibisawala) amefunguka sababu zilizompelekea kusaini kandarasi jipya ndani ya Simba siku litakalomweka klabuni hapo hadi mwaka 2028.

Mpanzua na viongozi wa Simba

Kupitia ujumbe wenye hisia, Mpanzu amekiri kuwa mapenzi ya mashabiki wa Simba ndiyo yaliyomfanya akatae ofa nyingine na kuchagua kubaki nyumbani.

"Nikiwa na machozi machoni, ninawaandikia,  Ninyi ndio wafuasi bora zaidi ambao nimewahi kukutana nao," ameandika Mpanzu, huku akishukuru kwa maombi na sapoti ya mashabiki iliyomsaidia kurejea kwenye kiwango chake bora baada ya kupitia kipindi kigumu.

Mkongomani huyo amesisitiza kuwa uamuzi wake wa kuongeza mkataba ni sehemu ya shukrani kwa mashabiki waliomwamini: "Nimeamua kutowasaliti na kuendelea na klabu. Ninawapenda nyote na nawaahidi mambo mema."