wasanii katika uzinduzi wa kampeni ya 'Bwela Kuni'
'Bwela Kuni', neno la kingoni ambalo lina maanisha njoo hapa, ni kazi ambayo imefanyika chini ya mtayarishaji muziki C9 Kanjenje ambaye ndiye muasisi wa wazo hilo, na hapa anazungumza kwa niaba ya wenzake anaeleza umuhimu wa kazi hii katika kuwainua wasanii wa Ruvuma.
Huu ni mwanzo wa project hii ambayo itahusisha pia wasanii kama vile Professor Jay, Mrisho Mpoto, Mtayarishaji muziki Mr T Touches ambao wote pia ni wanaotoka mkoa wa Ruvuma.