Jumatatu , 23rd Feb , 2015

Katika jitihada za kupambana na matukio ya kinyama ya Mauaji ya Albino nchini, Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiongozwa na Keisha wametengeneza rekodi maalum kusaidia kuongeza uelewa na kukemea ukatili huu dhidi ya walemavu wa ngozi.

Keisha

Kuhusiana na Project hii, inayokwenda kwa jina la Simama Nami, eNewz tumeongea na Keisha ambaye kwa hisia nzito amefafanua maana ya rekodi hiyo na kuwataka watanzania kila mmoja kwa nafasi yake kusimama na kupambana dhidi ya vitendo hivyo vya kinyama vya mauaji ya albino.

KEISHA.
Keisha amesema kuwa, imamuuma sana na anakata tamaa na nchi yake kila siku zinavyozidi kwenda. “Natamani niiikimbie hii nchi niende mbali ambapo labda sitoweza kushuhudia huu ukatili unaoendelea ndani ya nchi mnayoiita nchi yenye amani.”