Jumanne , 9th Apr , 2024

Kwa mujibu wa rapa Wakazi anasema mwanaume kujua kupika ni kitu kizuri na ujuzi muhimu unaopunguza utegemezi pia mwanamke anapenda mwanaume anayeweza kupika.

Picha ya rapa Wakazi

“Mwanaume kujua kupika ni kitu kizuri, Ni ujuzi muhimu wa maisha unaopunguza utegemezi na unajua mwanamke anapenda mwanaume anayeweza kupika”

“So mcheke Lunya halafu uje kuta kampikia demu wako “Mbuzi” na kamla, Pia wapishi wengi maarufu duniani ni wanaume! Exposure tatizo” ameandika Wakazi

Wakazi amefunguka hilo baada ya Interview aliyofanya #Tundaman akimsifu #YoungLunya kuwa ni anajua kupika na mpishi mzuri.