Alhamisi , 8th Sep , 2022

Katika kuhakikisha sasa ubora wa burudani unarudi kwao waanzilishi hii leo Septemba 8, 2022, kampuni THE WORKS kwa kushirikiana na East Africa Television na East Africa Radio wamesaini mkataba kwa ajili ya kuandaa na kusimamia matukio mbalimbali ya burudani.

Wawili kushoto ni watangazaji wa East Africa TV&Radio Bhoke na Dullah Planet, katika ni Careen Maro kutoka EATV na Ahmed Yusuph kutoka THE WORK wakisaini mikataba hiyo na wa mwisho kulia ni Shumensa Nassor kutoka THE WORK

Ushirikiano ulioingiwa hii leo na taasisi hizo mbili ni wa miaka miwili mfululizo watu wakikata kiu ya burudani ukihusisha uandaaji na usimamizi wa matamasha yote ambayo yatakuwa yanaratibiwa na East Africa Television na East  Africa Radio hapa nchini Tanzania.

Hata hivyo mwakilishi kutoka EATV amesema ushirikiano huo imefungua ukurasa mpya katika burudani.

THE WORKS imekuwa na uzoefu wa hali ya juu katika uandaaji wa matukio mbalimbali ya burudani huku East Africa Television East Africa Radio na mitandao yetu ya kijamii ikiwa na uzoefu wa kuibeba burudani hivyo sasa kuwataka Watanzania na wapenda burudani kujitokeza kuchukua tiketi katika tukio la kwanza kubwa litakalofanyika Ware House, Next Door Masaki Dar es Salaam.

Kauli mbiu yetu ya kiburudani zaidi inasema kwamba 'Kila kitu kwa mara ya kwanza”