Alhamisi , 17th Dec , 2015

Muigizaji na muongozaji wa filamu toka Marekani Vin Diesel ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na filamu ya Fast & Furious, amepata dili lingine kubwa la kutengeneza muendelezo wa filamu yake ya Riddick ambayo ilitoka mwaka 2013.

Vin Diesel amesain mkataba huo jumatano ya wiki hii wa kufanya kazi na Universal, ambapo kitu cha kwanza anachotarajia kukifanya ni kutengeneza muendelezo wa filamu ya Riddick (series) ambayo anataka kuiita Merc City.

Mkataba huo wa Diesel na Universal ni wa muda mrefu ambao utaipa fursa kampuni ya Vin Diesel ya One Race, kupitia kwa mara ya kwanza na kuzitolea maoni filamu zinazotengenezwa kabla hazijaachiwa rasmi.

Kampuni ya One Race ilianzishwa mwaka 1995 na imetengeneza filamu 12, ikiwemo filamu tatu za Fast & Furious, na mbili zikiwa za Riddick, pamoja na nyingine ambayo inatarajia kufuata ya Riddick.

Ni muda tu ndio utakaojibu kama Universal watavunja mkataba na Diesel, lakini kitu cha kuaminika ni kwamba Vin Diesel atatakiwa kugawanya mtazamo wake kati ya kazi zake.

Vin Diesel kwenye movie ya Riddick