Jumatatu , 21st Jul , 2014

Vijana wa kitanzania kutoka Umoja Cultural Flying Carpet nchini Tanzania wanatarajia kwenda kuweka kambi nchini Ethopia kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika tamasha la umoja Cultural Flying Carpet kimataifa.

Mwanamuziki Carola Kinasha wa nchini Tanzania

Akiongea na eNewz Matron wa vijana ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini Carola Kinasha, amesema lengo ni kuwakuza vijana na vipaji ambapo wataweza kuwaleta pamoja vijana wa mataifa tofauti kuweza kutunga kitu kimoja wakihusisha vipaji vyao.

Vijana hao wanatarijia kukutana na vijana wenzao wa Afrika Mashariki katika kambi itakayo kuwa nchini Ethiopia ambayo itazishirikisha nchi kama Tanzania, Kenya, Uganda, na Ethiopia yenyewe.

Carola ameongezea kuwa baada ya kambi hiyo watachaguliwa vijana kadhaa na kuweza kuiwakilisha Afrika Mashariki katika tamasha kubwa zaidi la kitaifa ambalo litazihusisha nchi za Msumbiji, Zimbambwe na Afrika Kusini pia na bara la Ulaya litawakilishwa na nchi za Norway na Uholanzi.