
QS Mhonda akiwa na Q Chillah
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, msanii huyo alionekana mwenye furaha kubwa baada ya kupokea taarifa ya kuruhusiwa kutoka ndani ya QS J Mhonda.
“Napenda nitangulize shukrani zangu za dhati kwa yote uliyonitendea, ushirikiano wako na utendaji wako wa kazi umenisaidia, kuniimarisha na kunijenga kisaikolojia”. Baadhi ya maneno aliyoandika Q Chief katika barua yake ambayo imekwenda kwa Muhonda
Aidha Chillah alisema kilichompelekea yeye kuandika barua hiyo ni kutaka kumshukuru aliyekuwa muajiri wake kwa mema na mazuri yote aliyomfanyia pindi alipokuwa katika kampuni hiyo.
Kwa upande mwingne msanii huyo hakutaka kuzungumza lolote kuhusiana na tetesi zilizoenea kuwa Mb Dogg nae pia ametoka katika ‘Lebo' ya QS J Muhonda’ na kutaka swali hilo atafutwe mwenyewe aweze kufafanua sababu za kuondoka.
Q Chillah
“Unapaswa ujiulize kwanini hawajaondoka kabla ya mimi kuondoka, ‘I did it for my future’ lakini kama wanahisi mimi nimekuwa mfano wa kutambua matatizo yao basi wanaweza wakafanya vile wanavyojisikia ila kama hawana uhakika na wanachotaka kukifanya wasikurupuke wajipange”. Alisisitiza Q Chief
Hata hivyo msanii huyo alisema kila ambaye anatoka katika kampuni hiyo ana sababu zake binafsi hawawezi wote wakawa sawa.
Itazame hapa...