Alhamisi , 31st Dec , 2020

Staa wa Tanzania aliyetangaza kuacha muziki Vanessa Mdee, amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Rotimi ambaye ni msanii wa filamu na mwanamuziki Rotimi ambao wanaishi wote kwa sasa nchini Marekani.

Kushoto ni Vanessa Mdee na Rotimi kulia ni pete ambayo amevalishwa Vanessa Mdee

Kupitia 'videos clip' ambazo zimepostiwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha Rotimi akiwa amepiga magoti mbele ya Vanessa Mdee huku akimvalisha pete hiyo ya uchumba, kisha wakakumbatiana na kuanza ku-kiss.

Ikumbukwe tu mwanzoni mwa mwezi wa kumi mwaka 2020, Vanessa Mdee na Rotimi walishea picha mitandaoni zikiwaonyesha wamechorana 'tattoo' zenye majina yao kwenye miili yao.

Penzi la wawili hao lilianza Oktoba 2019, baada ya Vanessa Mdee kuachana na mkali wa RnB Bongo Juma Jux ambao walidumu kwa miaka 6.