Jumatatu , 23rd Mar , 2015

Kifo cha msanii wa muziki AK47 wa nchini Uganda, kimeendelea kuzua maswali hasa kutokana na taarifa mpya kuibuka kuwa, baunsa aliyeibuka na kuandika maelezo polisi kuhusiana na namna alivyomkuta marehemu baada ya kuanguka na kuzimia, siyo mwenyewe.

msanii wa muziki wa nchini Uganda marehemu AK47

Taarifa hizo mpya zimetolewa na mhudumu aliyekuwa eneo la tukio siku ya kifo cha marehemu, taarifa ambazo zinaongezewa nguvu na ripoti ya msanii Diamond Oscar aliyekuwa na marehemu siku ya tukio kuwa, waliletewa taarifa ya kuanguka na kuzimia kwa marehemu na baunsa ambaye hawamfahamu.

Sambamba na hisia kuwa huenda marehemu alishambuliwa na kuumizwa kabla ya kufariki, imefahamika kuwa Jumamosi iliyopita, marehemu aliingia katika ugomvi na mabaunsa katika baa nyingine iliyopo maeneo ya Cemetery Park huko Uganda.