kundi la The Winners la shindano la Dance100% 2014
Kundi hili lenye vipaji vya aina yake katika sanaa ya kudansi, limeiambia eNewz kuwa wanajiamini na wana uhakika na wanachokifanya kutokana na aina ya mashindano ya mwaka huu yalivyo kwani hadi kufikia hatua ya nusu fainali uwezekano wa kujishindia shilingi milioni 5 upo pale pale.
Siku ndiyo zinaendelea kukata, na macho yote ni kuelekea fainali za mashindano haya, swali lenye uzito wa kutosha likibaki kuwa ni kundi gani litakalochomoka na mpunga wa milioni 5 kati ya The WT, Wakali sisi, Best Boys, Wazawa Crew na The winners Crew.