Jumanne , 21st Apr , 2015

Kundi maarufu la wasanii wa muziki nchini Rwanda 'The Urban Boyz' wameweza kukamilisha ndoto zao za kufanya kolabo na nyota wa Nigeria Timaya wakati walipotumbuiza hivi majuzi mjini Lagos nchini Nigeria.

wasanii wa kundi la 'Urban Boyz' wa nchini Rwanda

The Urban Boyz' wameelezea kufurahia kufanya colabo hiyo na mkali huyo kwani ni njia mojawapo ya kujitangaza na kupata soko zaidi kimataifa kupitia nyimbo na maonesho yao ya muziki.

Hii ni mara yao ya pili kufanya kazi na nyota wa nchini Nigeria kwani mwaka jana walifanya colabo na Iyanya na wamewasihi mashabiki wao kuwa kazi hiyo na Timaya itakuwa ni ufunguzi mpya kuliiteka soko la Afrika.