Msanii wa BongoFleva MB Dogg
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital kuhusu ukimya wake MB Dogg amesema kazi ya muziki haiwezi akiwa peke yake hivyo anahitaji msaada, sapoti na pesa.
"Biashara ya muziki imekuwa na changamoto kubwa ambapo watu wanawekeza sana kwenye kuwezesha, ukijikuta upo mwenyewe halafu una mipango mingi itabidi utafute watu wakukingie kifua, sapoti na pesa ambayo inahitajika japo sio sana ila ndiyo kikwazo kikubwa kingine ni nguvu na akili"
Aidha MB Dogg ameongeza kusema kuna harakati ambazo anazifanya kwa sasa zinazosababisha kuhama mji na sasa hivi anafika hadi boda ya Holoholo ambapo ni mpakani mwa Tanzania kuingia Mombasa, Kenya ili kukamilisha shughuli hizo.