Jumatano , 6th Mei , 2020

Mtangazaji wa show ya 5Selekt ya East Africa TV  TBway 360, amesema anahitaji tuzo za kumvumilia mpenzi wake Kim Nana kipindi cha ujauzito wake, kwani alikutana na changamoto nyingi na aliweza kuzishinda.

Mtangazaji T-Bway 360 na mpenzi wake Kim Nana

Akizungumzia kuhusu mahusiano yake na Kim Nana, kipindi cha ujauzito hadi kuwa mzazi kwenye kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio,inayoruka kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 4:00 Asubuhi - 6:00 Mchana, TBway amesema,

"Kim Nana siyo Slay Queen, nilianza naye mahusiano muda mrefu sana kama miaka mitano au sita iliyopita, kabla hata ya Instagram haijapamba moto au kuwa na kiki, tulipanga kuwa na mtoto, muda ulipofika tulifanya hivyo japo mwanzoni tulikuwa tunaogopa" amesema T-Bway.

Aidha ameendelea kusema  "Kama kuna mwamba aliyevumilia kipindi cha ujauzito basi ni mimi, kuna usiku mmoja alinipigia simu anataka Pizza nikamwambia namtuma mtu au watu wa "Delivery" walete akakataa hadi nikampelekea mwenyewe ila cha ajabu naamka asubuhi hakula hata moja".

"Ilitokea ujauzito wa kwanza tukaenda Hospitali, kuangalia kwenye vipimo haionekani, Daktari akasema tusubiri kama wiki 2, tukirudi nyumbani anaonyesha dalili zote za kuwa mjamzito nikaona ananidanganya hadi tukagombana, nilijua mimi ndiyo tatizo" ameongeza.