Jumatatu , 22nd Jun , 2015

Joseph Mbilinyi ' Sugu' amemfikisha kortini aliyekuwa mkewe, Faiza Ally, akitaka apewe mtoto wao, Sasha mwenye umri wa miaka miwili, amlee maana mama yake si muadilifu.

Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akiwa Bungeni

Kwa mujibu wa taarifa, Sugu alimueleza hakimu mfawidhi wa mahakama, Patrick Vaginga, kuwa mbali na mzazi mwenzake huyo kuwa na tabia ya kuvaa nusu utupu pia ana mtindo wa kupiga picha zisizo na maadili na kuziweka mtandaoni yeye mwenyewe, sababu nyingine ikiwa ni kipato kidogo na safari za mara kwa mara za mwanadada huyo ambazo humwacha mtoto bila mlezi.

Kwa upande wa Faiza katika utetezi wake amedai muheshimiwa huyo hafai kumlea mtoto wao kwasababu naye ana tabia ya kusafiri kwa muda mrefu hivyo kuishi mbali na mtoto ambapo aliiomba mahakama hiyo isimruhusu baba mzazi huyo kuishi na mtoto kwa kuwa atamharibu.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka baadaye mwezi huu ambapo hukumu itatolewa.

Kivazi kilichomuweka Faiza katika vichwa mbalimbali vya habari hivi karibuni kutoka zulia jekundu za tuzo za mwaka huu za Kili
Faiza akiwa na mwanae Sasha
Aina ya mavazi tata ya Faiza