Alhamisi , 20th Feb , 2014

Wasanii wenye uwezo mkubwa kabisa wao nchini Kenya, STL, Kanja pamoja na Shreekeezy, wameamua kuonyesha mapenzi yao kwa Jiji la Nairobi, kwa kuungana pamoja na kufanya ngoma ambayo inakwenda kwa jina For My City.

Katika ngoma hii kali, wapo pia wasanii Roberto na Juliet Ibrahim vilevile kutoka huko nchini Kenya, na wote kwa pamoja wameweza kuonyesha uwezo mkubwa wa kufanya michano katika mitindo tofauti tofauti.

Kivutio kikubwa katika ngoma hii, ni wazo la kutengeneza kitu kwa ajili ya kuonyesha umuhimu na mapenzi ya sehemu ambayo ndiyo chimbuko la mastaa hawa mahiri kabisa katika game ya muziki Afrika Mashariki.