Jumamosi , 30th Aug , 2014

Rapa Stereo ambaye ameachia kwa mashabiki wake kolabo yake ya Kimataifa, "Wako", featuring Victoria Kimani, ameweka wazi sababu za kazi hii kuchelewa kuachiwa, ambapo amesema kuwa ni kutokana na Video ya Usione Hatari kuchelewa kutoka.

Victoria Kimani na Stereo

Stereo amesema kuwa, aliamua kutoa muda kwa kazi yake hii iliyotangulia, Usione Hatari kuwakaa mashabiki wake kabla ya kuwahamishia katika jiwe jingine, Wako ambalo tayari limepokelewa vizuri mitaani na mashabiki wa muziki.

Kuhusiana na video ya kazi hii mpya ya kimataifa, Stereo amesema kuwa baada ya wiki mbili tatu, atakuwa ameweka mambo kwenye mstari.