Jumatatu , 20th Apr , 2015

Baada ya kutoka kwa ngoma inayokwenda kwa jina Ukonga na Ilala Rapa Stereo ambaye mwishoni mwa wiki aliitambulisha kazi hiyo rasmi kupitia East Africa Radio amesema kuwa, kwa muda mrefu alikuwa na ndoto za kufanya kazi na Chidi Beenz.

rapa Stereo wa nchini Tanzania

Stereo amesema kuwa, kukamilika kwa kazi hiyo na kufanya kazi na Chid ni kukamilika kwa ndoto yake ya muda mrefu, akisisitiza pia kuwa mpango wa kufanya video ya kazi hiyo upo, wakiwa sasa wamejikita katika kuisambaza rekodi yenyewe kwanza.