
Stara amesema kuwa, anakumbuka mwaka 2005 alimsaidia Mheshimiwa Sugu kufanya kiitikio katika rekodi yake, ambapo aliongozana naye studio licha ya kuwa alikuwa ndio ametoka kujifungua mtoto wake wa pili, akionelea kuwa anastahili heshima zaidi kutoka kwa mwanasiasa huyo.
