Jumatatu , 4th Jul , 2016

Msanii wa Bongo Flava Judith Wambura maarufu kama Komandoo Lady Jaydee amesema kwamba hawezi kumhukumu mtu yeyote katika kazi zake za usanii kwani mashairi yake anayoimba ni kiswahili fasaha kinachoeleweka.

Jaydee ameyasema hayo kwenye kipindi cha EABREAKFAST alipokuwa akizindua wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'Sawa na Wao' ambao anazungumzia maisha halisi katika jamii huku ukiwa na lugha ya kiswahili na kikongo katika mahadhi ya lingula.

Jaydee amesema kwamba wimbo huo ameurekodi disemba mwaka jana na imani yake ni kwamba hata waangusha mashabiki katika kazi ambazo anazitoa na atakazozitoa.

''Idea imetokana na maisha ninayoishi, kila mtu ana tabia zake mimi nina tabia zangu na mwingine ana tabia zake lakini tukikutana tunakuwa wamoja'' Amesema Lady Jaydee.

Aidha ameweka wazi kwamba ziara ya Naamka tena inaendelea mikoani na anatarajia kufika mikoa yote nchini kwa kuwa mashabiki wake walimkosa kwa muda mrefu.