Jumatatu , 16th Feb , 2015

Meneja wa kundi la muziki la TMK Wanaume Family na Mkubwa na Wanawe Said Fella, amelalamika juu ya matapeli walioibuka katika siku za hivi karibuni na kutumia jina lake kurubuni wananchi kujipatia fedha.

Said Fella

Fella ametahadharisha watu wote wenye nia ya kufanya kazi naye, hususan wasanii chipukizi kuwa makini na watu hawa, akisisitiza pia kuwa hakuna malipo yoyote ambayo anatoza ili kuwaandikisha watu katika kituo chake cha mkubwa na wanawe.