Jumapili , 4th Oct , 2015

Baada ya kufanya vizuri kupitia projekti ya 'Sidanganyiki' akiwa amemshirikisha Juma Nature, Msanii wa muziki Riz Conc amejipanga kufungua wiki kwa ujio wa kishindo na rekodi mpya inayokwenda kwa jina 'Sitaki Shari'.

Msanii wa muziki Riz Conc akiwa na Sir Zulu katika kava ya wimbo wao mpya 'Sitaki Shari'.

Riz ameweka wazi katika rekodi hiyo mpya safari hii ameamua kumshirikisha staa wa bongo aliyekuwa akiishi huko Afrika Kusini, Sir Zulu.

AKiwa amebadilika kabisa kutoka katika michano kwenda katika kuimba, Riz Conc amesema kuwa ili kuwafikia pia mashabiki wa jinsia ya pili ameingia katika kuimba, huku akieleza kuwa amepata nafasi ya kufanya kazi na Sir Zulu kutokana na uzoefu wake katika game Tanzania na Afrika Kusini.