Jumamosi , 1st Aug , 2015

Mwanamuziki wa Kike Kutoka nchini Tanzania alietamba katika miaka ya 2000 na baadae kuangukia katika dimbwi la Utumiaji wa madawa ya Kulevya Ray C amesema soon baada ya kumaliza dozi yake atarudi rasmi kwenye muziki.

Ray C

Ray C mpaka sasa amesema amesharekodi nyimbo tisa ambazo anasubiri kuziachia baada ya kumaliza dawa hizo mnamo mwezi Desemba baada ya hapo atarudi rasmi game

Ray C amesema kwa sasa bado anaangalia ni management ipi anaweza kufanya nayo kazi ili aweze kuwafurahisha mashabiki wake waliommiss kwa muda mrefu.

Tags: