
Mdau wa muziki,Fredrick Bundala a.k.a Sky Walker,
Akizungumza kwenye Planet Boongo ya East Africa Radio, Sky Walker amesema kwa sasa watu wengi wa nje ya Tanzania wanajua Tanzania ina wasanii wengi wa kuimba, kwani hawawajui rappers waliopo bongo kitu ambacho kinawafanya wanakosa fursa zingine.
Sky Walker amesema kwa sasa wasanii hao wanatakiwa kujitangaza kwa kufanya 'media tour' kama ambavyo wasanii wa nchi nyingine wanavyofanya kwa kuja Tanzania na kutangaza kazi zao, ingawa ni jambo gumu lakini ni lazima lifanyike, kwani kutoa wimbo au video nzuri haitoshi kwa msanii kujitangaza kwenye nchi zingine
"Imefika stage kwamba kama watu wa Afrika Kusini, Nigeria hawaijui Tanzania kama ni nchi ambayo inafanya vizuri kwenye hip hop, kwa sababu hata wasanii ambao wamekuja ukiwauliza nani ambaye wanamjua, kwa mtazamo wa watu wa nje sasa hivi kwa Tanzania, ni kwamba Tanzania ni nchi ina waimbaji zaidi kuliko rappers", alisema Sky Walker.
Wasanii wa hip hop wa Tanzania wamekuwa wakishutumiwa kutofanya vizuri na kushindwa kufika kimataifa, hata kukosa fursa za kuwekwa kwenye tuzo za kimataifa tofauti na wasanii wa kuimba.
Msikilize Sky Walker hapa chini alichokizungumza kuhusu wasanii wa hip hop kutojitangaza na nini wafanye ili kuupeleka mbali zaidi muziki wao.
Msikilize hapa:-