Jumatatu , 9th Nov , 2015

Rais wa Uganda, Mheshimiwa Yoweri Museveni ametenga muda wake na kuingia studio kuandaa rekodi inayosimama kwa jina Kwezi, ikiwa inaeleweka wazi kuwa hatua hiyo ni kwa ajili ya mbio za uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mapema mwaka ujao.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiwa na baadhi ya wasanii wa muziki

Kazi hiyo ambayo imekwishakamilika inabeba mashairi ya mheshimiwa akiwa anazungumzia chama chake tawala cha NRM na mafanikio ambayo ameyapata katika uongozi wake, tayari kabisa kwa kuingia mtaani kuburudisha mashabiki na kumuongezea idadi ya wapiga kura hususan wale wapenzi wa muziki wake.

Rekodi hii ya Rais Museveni inakuwa ni ya pili kutoka, ikiwa imetayarishwa kwa ushirikiano na producer Washington ambaye alipata nafasi ya mualiko maalum Ikulu kwa ajili ya kutengeneza na kurekodi mdundo huo mpya wa Museveni.