Msanii Madee.
Madee ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo idadi kubwa ya wasanii wakubwa wa nchini kukimbizana kuachia kazi zao mpya za muziki ambapo tokea mwezi Juni mpaka leo Julai 7, miongoni mwa wa wasanii ambao wametambulisha nyimbo hizo ni Ray C, Kundi la Weusi, Chege, Mr. Blue, Rama Dee, Young Killer, Nay wa Mitego, Chid Benz, na Timbulo.
"Radio na Tv zinazidiwa na utitiri wa nyimbo mpya zinazotoka kila siku, 'so' kama msanii siyo mbunifu usilalamike unabaniwa", ameandika Madee kupitia ukurasa wake wa twitter.
Pamoja na hayo, kuna nyimbo za wasanii mbalimbali zilizoachiwa hivi karibuni zimeshindwa kufanya vizuri katika vituo vya redio na luninga kutokana na nyimbo hizo kutokuwa na ubora na ubunifu jambo ambalo limepelekea 'ngoma' hizo kukosa muda wa kutosha na kushindwa kupambana.


