Wasanii wa nchini Uganda Mose Radio & Weasel
Hatua hii itawawezesha wasanii hawa kuwafikia tena mashabiki wao waliopo huko Ulaya ikiwa ni baada ya miaka 5 wakiwa wanapitiwa kando na dili zote za kwenda huko kwa ajili ya shughuli za muziki na binafsi.
Radio na Weasel waliwekewa zuio kuingia Ulaya mwaka 2009, na hii ni baada ya kukiuka sheria za uhamiaji walipokuwa na safari ya kwenda huko, ambapo walimlaumu promota aliyekuwa amewaandalia show kwa kuvunja taratibu hizo.