Alhamisi , 11th Jun , 2015

Quick Rocker, msanii wa muziki ambaye pia ni mtayarishaji muziki kupitia studio yake ya Switch, ameeleza kuwa katika kazi yake ya kutayarisha muziki, kitu kikubwa kinachomuhamasisha ni mudi nzuri ya furaha, na wakati mwingine kilevi kidogo.

msanii wa muziki wa bongofleva Quick Rocker

Quick Rocker ama Switcher kama anavyopenda kutambulika sasa, amesema kuwa kazi yake hususan ya kufanya shoo, huwa haifanyi akiwa ametumia kilevi kutokana na kujua kuwa hataifanya vizuri, isipokuwa wakati mwingine katika kufanya mixing ya rekodi, hutumia mambo kidogo kutengeneza mudi ya kazi.