Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi Joseph Haule 'Prof Jay'
Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mikumi amemtangaza Denis Lazaro wa CCM kuwa mshindi wa nafasi ya kiti cha Ubunge kwa kupata kura 31,411 sawa na asilimia 62.7 dhidi ya mpinzani wake Joseph Haule Prof Jay wa CHADEMA aliyepata kura 17,375 sawa na asilimia 34.7
Prof Jay ameliongoza Jimbo la Mikumi kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kushinda kwenye Uchaguzi uliopita mwaka 2015.