Jumanne , 3rd Aug , 2021

Ni headlines za msanii wa Dullah Makabila ambaye amesema kwa mke wake Rahima ana uwezo wa kutumia pesa yoyote na hata akiwa na milioni 3 basi anaweza kutumia milioni 2 kubakisha milioni 1 na vitu hivyo ni vya kawaida sana kwa upande wake.

Picha ya Dullah Makabila na mkewe Rahima

"Mimi nafanya kazi sio king'asti, mfukoni nina mzigo wa kutosha nipo vizuri, kwa mke wangu natumia pesa yoyote kwenye milioni 3 halafu kubaki na milioni 1 ni vitu vya kawaida sana kwangu, yaani baada ya kumuoa Rahima movement zangu za show zimefunguka tofauti na mwanzo, watu wasitegemee mambo mengine sasa hivi nimetulia" ameeleza Dullah Makabila 

Pia Dullah Makabila amesema kuna baadhi ya vitu anavijutia kuvifanya kabla ya kuingia kwenye ndoa na sasa hivi ndoa imembadilisha kwa vitu vingi kuanzia mipango, baraka na heshima.

Zaidi mtazame hapo chini kwenye video.