Ijumaa , 8th Oct , 2021

Nyota wa muziki wa RnB kutoka Kenya, Otile Brown amepata pigo kubwa baada ya video zake zisizopungua nne kuondolewa kwenye mtandcao wa YouTube siku za hivi karibuni.

Picha ya Msanii Otile Brown

Nyimbo zilizofutwa ni pamoja na Dusuma, Chaguo La Moyo, Aiyana na Such Kinda Love ambazo kwa pamoja zilikuwa zimevuna zaidi ya watazamaji (viwers) Milioni 10 na kumpa mafanikio makubwa katika historia ya muziki wake huku akielezea masikitiko yake kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa yeyote aliyehusika.