Alhamisi , 28th Sep , 2017

Msanii Ommy Dimpoz ambaye hivi karibuni ameachia 'video' yake mpya ya 'Cheche' amekanusha taarifa za kuwa na mtoto nchini Marekani, na kusema kwamba bado hajajaliwa kupata mtoto kabisa.

Ommy amezungumza kwenye eNewz ya East Africa Television, baada ya kuulizwa  kuhusu mtoto ambaye amekuwa akimpost kwenye instagram, kusema mtoto huyo siyo wake licha ya kuwa wanafanana.

"Mimi sina mtoto  kwa kweli yule ni mtoto wa rafiki yangu, kwa hiyo mimi kwake ni kama baba. Sema nilivyopost na unajua sura zetu kidogo kama zinafanana, watu wakasema mtoto wa Dimpoz, mimi siwezi kujisingizia lakini kama Mungu akijaalia kama wangu atakuwepo wala sitaleta kona kona nitasema jamani mtoto wangu huyu", amesema Ommy Dimpoz

Hivi karibuni Ommy Dimpoz alipost picha akiwa na mtoto mdogo wa kike na baadhi ya watu wakidai ni wake lakini cha kushangaza msanii huyo aliifuta picha ya huyo mtoto ambaye ilikuwa katika ukurasa wake na kuacha video moja inayomuonyesha yuko naye na kuzima kitufe cha maoni 'comment'.